Staa wa muziki nchini, Ben Paul amerejea tena kwenye vichwa vya habari, safari hii ikiwa ni kutokana na hatua yake ya kuamua kubadili dini na kuwa Muislamu.

Hii inajiri baada ya kuwepo kwa gumzo mitandaoni juu ya kile kinachoendelea kwenye ndoa yake na baadhi ya wadaku wakidai kuwa hali si shwari kwa Mwana RNB huyo.

BenHam

Ben Pol ambaye kwa sasa jina lake ni ‘BenHam’ ame-share picha kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram, zikimuonesha akiwa Msikitini akislimu na kuambatanisha na maneno yaliyosomeka…

“BISMILLAH-HIR-RAHMAN-NIR-RAHIM. 23.10.2020” – ameandika BenHam.

Mashabiki zake wengi wakiwemo mastaa wakubwa Bongo kama Dioamond Platnumz, Fid Q wamenyesha kumuunga mkono mkali huyo wa RNB. Na kama kawaida mtandaoni wapo wanaopinga na kudai kuwa ni kiki.

BenHam


vumbi_la_kongo_mbeya

Bongo bila kiki hutoboi….utashangaa yupo location…


angel_unusual

Hiii itakuwa nyimbo lazima


appletz1

Anahangaika tu kesho kutwa kwa mwamposa kukanyaga mafuta


ummu_raniya

Dini sio kitu cha kuchezea jamani km upo radhi bac karibu ktka uisalamu

Wakati hayo yakijiri baadhi ya mashabiki zake walivamia mtandao wa Instagram kwenye ukurasa maalumu wa Anerlisa ambae ni Mke wake na kumshushia lawama za kuvua pete na usaliti wa BenHam.
Anerlisa

dessy.kiWifi umevua Pete ya Kaka Ben why

  • ubunifutofautitofauti@dessy.ki ben uyo amebadilisha dini uko mschexxxx mwache anerlisa wangu kaepuka mengi

  • smaudaku@ubunifutofautitofauti hila Ben aeleweki heeeh wanaume ni kazi kweli na huyu dada kamsitili sana pol sio bule nimekasilika kwa kweli huyu dada ni mzuri walikuwa wanaendana sasa nini tena